Zoezi la Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga maarufu ‘Women With Vision’ kukabidhi misaada ya vitu mbalimbali kwa ajili ya wanawake waliopo katika Gereza la Wilaya ya Shinyanga likiendelea.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga maarufu ‘Women With Vision’ kimeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa misaada ya vitu mbalimbali kwa wanawake waliopo katika Gereza la Wilaya ya Shinyanga pamoja na watoto waliozaliwa kabla ya muda katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wanawake hao wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba wametembelea Gereza la wilaya ya Shinyanga na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Machi 8, 2021.
Mbunge Santiel Kirumba amesema ameamua kuambatana na wanawake hao na kutembelea wanawake katika gereza na hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
“Tumeona wanawake katika gereza la wilaya ya Shinyanga wamepewa ujuzi wa aina mbalimbali, wanajishughulisha na ujasiriamali hali itakayowasaidi kuingiza kipato hata baada ya kutoka gerezani na tumeona wanaishi maisha ya furaha kuliko hata sisi tulio nje ya gereza”,amesema Mhe. Kirumba.
“Tumewatia moyo pia wanawake waliojifungua watoto ambao hawajafikisha muda wa kuzaliwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga ili kuwatia moyo wanawake hawa. Nimefurahi jinsi watoa huduma za afya wanavyotoa huduma vizuri”,ameongeza Mhe. Kirumba.
Katibu wa Kikundi cha Women With Vision, Abigaeli Hamis na Mwenyekiti wa kikundi hicho Winfrida Mlimandago wamesema wameamua kusherehekea Siku ya wanawake duniani kwa kuwatembelea na kuwafariji wanawake waliofungwa katika gereza la wilaya ya Shinyanga na kuwapatia zawadi mbalimbali zikiwemo sabuni na taulo za kike.
Aidha wamesema kwa upande wa hospitali ya rufaa mkoa wa Shinyanga wamewatembelea akina mama waliojifungua watoto waliozaliwa kabla ya muda pia zawadi ya taulo za kike, pampers, panty liners, mafuta,sabuni ili ziwasaidie wakati wakiendelea kupata huduma za afya katika hospitali hiyo.
“Tumetembelea wanawake waliopo katika gereza la wilaya ya Shinyanga na kuonana na wanawake ambao wanajishughulisha na shughuli za ujasiriamali wa aina mbalimbali ikiwemo kutengeneza mazulia mazuri”,amesema Katibu wa Kundi la Women With Vision Abigael Hamis.
Naye Mkuu wa Gereza la wilaya ya Shinyanga sehemu ya Gereza la Wanawake ASP Grace Thomas Massawe amekishukuru kikundi cha Women With Vision kwa kutembelea gereza hilo na kuwapatia wafungwa wanawake mahitaji muhimu zikiwemo taulo za kike, panty liners na sabuni.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Justina Nkinda pia ameeleza kufurahishwa na kitendo cha wanawake hao ‘ Women With Vision’ kutoa misaada kwa watoto waliolazwa na watoto waliozaliwa kabla ya muda katika hospitali hiyo.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Gereza la wilaya ya Shinyanga sehemu ya Gereza la Wanawake ASP Grace Thomas Massawe boksi lenye sabuni kwa ajili ya wanawake waliopo katika gereza la wilaya ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake leo Jumatatu Machi 8,2021. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Gereza la wilaya ya Shinyanga sehemu ya Gereza la Wanawake ASP Grace Thomas Massawe boksi lenye sabuni kwa ajili ya wanawake waliopo katika gereza la wilaya ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake leo Jumatatu Machi 8,2021.
Zoezi la Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga maarufu ‘Women With Vision’ kukabidhi taulo laini kwa ajili ya wanawake waliopo katika Gereza la Wilaya ya Shinyanga likiendelea
Muonekano wa Taulo laini na Panty Liners za Flowless zilizotolewa na Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga maarufu ‘Women With Vision’ kwa ajili ya wanawake waliopo katika Gereza la Wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa Taulo laini, sabuni na Panty Liners za Flowless zilizotolewa na Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga maarufu ‘Women With Vision’ kwa ajili ya wanawake waliopo katika Gereza la Wilaya ya Shinyanga
Katibu wa Kikundi cha Women With Vision, Abigaeli Hamis akizungumza wakati Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga maarufu ‘Women With Vision’ kikikabidhi sabuni,taulo laini na panty liners kwa ajili ya wanawake waliopo katika Gereza la Wilaya ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Kikundi cha Women With Vision, Winfrida Mlimandago akizungumza wakati Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga maarufu ‘Women With Vision’ kikikabidhi sabuni,taulo laini na panty liners kwa ajili ya wanawake waliopo katika Gereza la Wilaya ya Shinyanga
Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza akiwa ameshikilia zulia lililotengenezwa na mmoja wa wanawake katika gereza la Wilaya ya Shinyanga wakati Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga maarufu ‘Women With Vision’ kikikabidhi sabuni,taulo laini na panty liners kwa ajili ya wanawake waliopo katika Gereza la Wilaya ya Shinyanga
Mkuu wa Gereza la wilaya ya Shinyanga sehemu ya Gereza la Wanawake ASP Grace Thomas Massawe akizungumza wakati Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali katika Manispaa ya Shinyanga maarufu ‘Women With Vision’ kikikabidhi sabuni,taulo laini na panty liners kwa ajili ya wanawake waliopo katika Gereza la Wilaya ya Shinyanga
Mwakilishi wa Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Justina Nkinda (katikati) akiwakaribisha Wana Kikundi cha Women With Vision waliofika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kutoa zawadi ya taulo laini,sabuni, pampers, panty liners na mafuta kwa ajili ya watoto waliozaliwa kabla ya muda katika hospitali hiyo.
Mwakilishi wa Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Justina Nkinda akiowaongoza wanakikundi cha ‘ Women With Vision’ kuelekea wodini kwa ajili ya kutoa misaada kwa watoto waliolazwa na watoto waliozaliwa kabla ya muda katika hospitali hiyo.
Wanakikundi cha Women With Vision wakiwa ndani ya wodi ya wanawake waliojifungua kawaida katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Muonekano wa maboksi yenye taulo laini, pampers, sabuni, mafuta kwa ajili ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kutoka Women With Vision
Mwakilishi wa Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Justina Nkinda (kulia) akiwa na Wana Kikundi cha Women With Vision wakiingia katika moja ya vyumba katika wodi ya wanawake waliojifungua watoto kabla ya muda kwa ajili ajili ya kutoa zawadi ya taulo laini,sabuni, pampers, panty liners na mafuta kwa ajili ya watoto waliozaliwa kabla ya muda.
Wana Kikundi cha Women With Vision wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga (katikati) wakimkabidhi mmoja wa wazazi zawadi ya taulo laini,sabuni, pampers, panty liners na mafuta
Wana Kikundi cha Women With Vision wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga (katikati) wakimkabidhi mmoja wa wazazi zawadi ya taulo laini,sabuni, pampers, panty liners na mafuta
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga, Mhe. Santiel Kirumba (kushoto) akizungumza ndani ya wodi ya watoto wakati kikundi cha Women With Vision wakikabidhi zawadi ya taulo laini,sabuni, pampers, panty liners na mafuta kwa watoto waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na watoto waliozaliwa kabla ya wakati katika hospitali hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga, Mhe. Santiel Kirumba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wazazi zawadi ya pampers kwa ajili ya mtoto.
Mweka hazina wa kikundi cha Women With Vision, Stella Mhondo akimkabidhi mzazi pampers kwa ajili ya mtoto aliyelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga, Mhe. Santiel Kirumba (katikati) na Katibu wa Kikundi cha Women With Vision, Abigaeli Hamis wakiendelea kukabidhi zawadi katika wodi ya watoto.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga, Mhe. Santiel Kirumba (katikati) akizungumza ndani ya wodi ya watoto
Mwakilishi wa Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Justina Nkinda akiowaongoza wanakikundi cha ‘ Women With Vision’ kuelekea katika wodi nyingine kwa ajili ya kutoa misaada kwa watoto waliolazwa na watoto waliozaliwa kabla ya muda katika hospitali hiyo.
Wanakikundi cha Women With Vision wakiwa nje ya wodi ya wanawake waliojifungua kawaida
Wanakikundi cha Women With Vision wakiwa wodini
Wanakikundi cha Women With Vision wakiwa wodini
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (kulia) akikabidhi pampers na taulo laini na panty liners katika wodi ya watoto
Katibu wa Kikundi cha Women With Vision, Abigaeli Hamis akikabidhi pampers wodini
Wana kikundi cha Women With Vision wakiwa nje ya wodi ya akina mama waliojifungua kawaida katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba akizungumza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Mwakilishi wa Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Justina Nkinda (kulia) akizungumza wakati wana kikundi cha Women With Vision wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto waliozaliwa na waliolazwa katika hiyo hiyo
Mweka hazina wa kikundi cha Women With Vision Stella Mhondo (kulia) akizungumza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa kikundi cha Women With Vision, Winfrida Mlimandago akizungumza katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Mwenyekiti wa kikundi cha Women With Vision, Winfrida Mlimandago akikabidhi boksi la Panty Liners Mwakilishi wa Mganga Mfawidhi hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Justina Nkinda (kulia).
Wana kikundi cha Women With Vision wakielekea katika wodi ya wagonjwa mahututi kwa ajili ya kutoa zawadi mbalimbali kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda
Wana kikundi cha Women With Vision wakiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga baada ya kukabidhi zawadi wodini
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog