BAO pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 86 limeipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya vigogo, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Azam Fc imefikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 28, ingawa inabaki ya tatu ikizidiwa pointi tatu na Yanga ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Mabingwa watetezi, Simba wanaendelea kutawala kileleni kwa pointi zao 58 za mechi 24.
Via Binzubeiry blog
Social Plugin