Spika wa Bunge Job Ndugai leo April 1, 2021 amewaapisha wabunge watatu walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wabunge hao ni Balozi Dkt. Bashiru Ally, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Balozi Liberata Mulamula ambao kwa pamoja wameapa mbele ya Spika wa Bunge.
Pia Spika Ndugai ametumia nafasi hiyo kuahirisha vikao vya Bunge hadi April 6 mwaka huu saa 3:00 Asubuhi na kuwatakia heri ya sikukuu ya Pasaka waumini wote wa madhehebu ya Kikristo.
Social Plugin