Wafanyakazi wa kiwanda cha Canon General Supplies Ltd cha utengenezaji wa Pombe ali wakiwa kwenye uzalishaji wa bidhaa hiyo kiwandani hapo, mara baada ya kuanza uzalishaji tena kutokana na kufungiwa mwaka mzima na Serikali.
Na Marco Maduhu, Shinyanga.
Wawekezaji wa viwanda Manispaa ya Shinyanga mkoani hapa, wamepongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa hotuba yake aliyoitoa hivi karibuni, wakati akiwapisha makatibu wakuu, na manaibu kutoka wizara mbalimbali, na kuonyesha neema kwa wawekezaji hasa kwenye suala la ulipaji kodi.
Wawekezaji wametoa pongezi hizo leo, wakati wakizungumza na waandishi wa habari walipotembelea kwenye viwanda vyao, kikiwamo cha utengezaji wa Pombe Kali cha Canon General Supplies, na uchakati wa mafuta ya kula cha Jielong Holdings Ltd.
Meneja msaidizi wa kiwanda cha Canon General Supplies Ltd Lazaro Simon, amesema kuwa Rais Samia ameonyesha matumaini makubwa kwa wawekezaji hapa nchini, kwa kuonya matumizi ya nguvu kwenye kudai kodi, bali itumike njia rafiki hali ambayo itasaidia kutofungwa kwa viwanda vyao, na kuendelea kulipa kodi kidogo kidogo hadi kumaliza deni.
“Sisi kama wawekezaji tunampongeza sana Mhe. Rais Samia kwa kuonyesha neema kwetu kwa kutuwekea mazingira rafiki ya kufanya biashara, na tunamuahidi hatutamuangusha, bali tunaendelea kulipa kodi kwa hiari yetu wenyewe ili kuongeza pato la taifa,”amesema Simon.
“Mfano mwaka jana kiwanda chetu hiki kilifungiwa na Serikali kwa masuala ambayo yalikuwa yanazungumzika, lakini tunamshukuru wamekifungulia na leo tumeanza uzalishaji, na sisi tulikuwa walipaji kodi wazuri tu, ukipiga mahesabu ndani ya mwaka mzima tuliofungiwa Serikali imekosa mapato Sh. bilioni 2.4,” ameongeza.
Aidha amesema kutokana na kufungiwa huko na sasa wameanza uzalishaji, imebidi wapunguze wafanyakazi 400 kutoka 500 na kubaki 100, kutokana na kupunguza kasi ya uzalishaji kwa sababu ya bidhaa zao kupotea sokoni.
Nao baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho akiwamo Ladslaus Dominic na Amina Shamte, wamesema masuala ya ufungiaji viwanda hayana afya hapa nchini, ikiwa vina sababisha upotevu wa ajira nyingi kwa vijana, na kuaza kuishi maisha magumu, na kutoa wito kwa Serikali pale penye changamoto wakae wazungumze.
Naye Kaimu Meneja wa kiwanda cha mafuta ya kupikia cha wawekezaji kutoka China (Jielong Holdings Ltd) Zhongjun Ji, amesema wanamuunga mkono Rais Samia kwa kurudisha matumaini kwa wewekezaji wakiwamo wa kigeni, ambapo walikuwa wameshakata tamaa kutokana na utumiaji wa mabavu kudai kodi.
Pia ametoa ushauri kwa Serikali kupitia wizara husika kupunguza mlolongo mrefu wa utoaji wa vibali vya kazi kwa raia wa kigeni wanaowekezaji hapa nchini, ili kuwapa fursa ya kufanya shughuli zao kwa uhuru.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Meneja msaidizi wa kiwanda cha Canon General Supplies Ltd cha utengenezaji wa Pombe kali Lazaro Simon, akizungumza na waandishi wa habari kiwandani hapo kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga.
Mfanyakazi wa kiwanda cha Canon cha utengezaji wa Pombe Kali Ladslaus Dominic, akizungumza na waandishi wa habari kiwandani hapo.
Mfanyakazi wa kiwanda cha Canon cha utengenezaji wa Pombe Kali Amina Shamte akizungumza kiwanda hapo.
Meneja msaidizi wa kiwanda cha Canon General Supplies LTD cha utengenezaji wa Pombe Kali Lazaro Simoni, akioyesha waandishi wa habari namna wanavyoendelea na uzalishaji wa bidhaa hiyo.
Wafanyakazi wakiendelea na uzalishaji wa Pombe Kali katika Kiwanda cha Canon General Supplies LTD.
Wafanyakazi wakiendelea na uzalishaji wa Pombe Kali katika Kiwanda cha Canon General Supplies LTD.
Wafanyakazi wakiendelea na uzalishaji wa Pombe Kali katika Kiwanda cha Canon General Supplies LTD.
Wafanyakazi wakiendelea na uzalishaji wa Pombe Kali katika Kiwanda cha Canon General Supplies LTD.
Wafanyakazi wakiendelea na uzalishaji wa Pombe Kali katika Kiwanda cha Canon General Supplies LTD.
Kazi ikiendelea ya utengenezaji Pombe Kali.
Wafanyakazi wakiendelea na kazi ya utengenzaji wa maboski kwa ajili ya kupakia bidhaa ya Pombe Kali.
Bidhaa ya Pombe Kali ikiwa kwenye Maboksi kwa ajili ya kuingia Sokoni.
Kaimu Meneja wa kiwanda cha mafuta ya kupikia cha wachina (Jielong) Zhongjun Ji, kulia akiwa na Mkalimani Khadija Yusuph kushoto, akielezea namna walivyoipokea hotuba ya Rais Samia kwa kutoa Neema kwa wawekezaji.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Social Plugin