Picha ya DMX enzi za uhai wake
Taarifa na vyanzo mbalimbali vya habari nchini Marekani vimeripoti kuhusu kifo cha msanii wa HipHop na Muigizaji Earl Simmons maarufu kama DMX ambaye hadi umauti unamkuta alikuwa na umri wa miaka 50.
DMX amefariki dunia siku ya leo Ijumaa April 9 katika Hospitali ya White Plains Hospital iliyopo Jijini New York, Marekani.
Chanzo cha kifo chake inasemekana kuwa ni kuzidisha matumizi ya madawa za kulevya na kupata mshtuko wa moyo, wiki iliyopita iliripotiwa kuwa alikimbizwa Hospitali kutokana na tatizo hilo.
Kwenye muziki msanii huyo alitamba na nyimbo kadhaa kama Get at me dog, Ruff ryders anthem, Money power respect, party up na kwenye upande wa kuigiza alicheza filamu kama Cradle 2 the grave, Belly, Never Die Alone, Beef, Beyond the law na nyinginezo.
Social Plugin