Na Mwandishi Wetu.
TAASISI ya ECLA Africa Consult yenye makao makuu yake Jijini Dar es Salaam, inayojihusisha na masuala ya ukaguzi, ushauri wa kifedha na kodi inatarajia kuendesha kwa vitendo mafunzo ya siku tano kwa wahasibu na wakaguzi kutoka NGO's, taasisi za Kidini na mashirika ya serikali.
Aidha mafunzo yatahusisha mbinu ya kuandaa taarifa za fedha (financial statements) kwa kutumia mfumo wa IPSAS (IPSAS framework).
Mafunzo hayo yameandaliwa kufuatia maamuzi ya Bodi ya wahasibu na wakaguzi, ya 22 June 2020 kubadili mfumo wa kuandaa taarifa za kifedha kutoka IFRS (International Financial Reporting Standards) kwenda IPSAS (International Public Sector Accounting standards) kwa NGOs, Taasisi za dini na Mashirika.
Akizungumza juu ya mafunzo hayo Meneja Ubia wa ECLA Africa Consult, Lauden Cheyo, alisema kuwa, mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia 12 Aprili hadi 16 Aprili, mwaka huu katika hoteli ya Regency Park , iliyopo Mikocheni Jijijini Dar es Salaam.
"ECLA Africa Consult, tayari tumefungua milango kuanzia Aprili Mosi mwaka huu kwa washiriki kujiunga na mafunzo haya kwa vitendo kwa kulipia kiasi cha Shilingi za kitanzania Milioni moja (Mil.1000000)" ,alisema Cheyo na kuongeza kuwa
"Nafasi bado zipo kwa mshiriki kuweza kulipia kupitia benki ya CRDB akaunti namba 0150554143800, jina la akaunti Ecla Africa Consult."
Aidha Cheyo alieleza kuwa, washiriki watapata wasaa wa kupata mafunzo hayo ya kibobezi na mwisho wa mafunzo hayo washiriki wote watatunukiwa vyeti maalum.
Aidha, washiriki pia wanaweza kuwasiliana na waandaji hao moja kwa moja kupitia mawasiliano yao +255762148095 ama +255713040994.
Pamoja na mambo mengine Cheyo alijinasibu kuwa Kampuni ya ECLA Africa Consult inaamini mafunzo hayo yataleta tija kwa washiriki kwa kuwawezesha kuandaa taarifa za fedha zinazokidhi viwango vya mfumo wa IPSAS.
Social Plugin