OCPD wa Thika Mohammed Kofa alisema jamaa huyo aliyetambuliwa kama Joseph Nyutu mwenye umri wa miaka 45 aliingia chumbani humo akiwa pekee yake Jumatatu, Aprili 26,2021 kulingana na ripoti ya The Standard.
Alisema kuwa awali ripoti zilionyesha kwamba aliaga dunia baada kunywa sumu lakini kiini haswa cha kifo chake kitadhibitishwa baada ya upasuaji wa maiti kufanywa.
Mwili wa marehemu ulipelekwa katika makafani ya hospitali ya Thika General Kago.
Hii sio mara ya kwanza kwa maafa kuripotiwa katika vyumba vya kukodisha vya kulala kwani awali kiliripotiwa kisa kingine ambapo jamaa mwenye umri wa makamo alipatakana ameaga dunia ndani ya lojing’i eneo la Maua, kaunti ya Meru.
Iliarifiwa kuwa marehemu alionekana akijivinjari na wanawake katika kilabu moja maarufu eneo hilo kabla ya kukodi chumba hicho cha kulala ambapo aliingia na warembo hao.
Watatu hao waliingia katika kilabu hiyo Jumanne, Januari 12 kabla ya mwanamume huyo kupatikana uchi akiwa ameaga dunia kitandani.
Wanawake hao walihepa lakini maafisa wa polisi waliofika eneo la tukio walipata mipira ya kondomu chumbani walimokuwa watatu hao.
Kwingineko mwanamume mwenye umri wa miaka 35 kutoka mtaani Dandora, Nairobi alizimia na kufariki dunia ghafla akila uroda na mpenziwe Jumatano, Januari 6.
Robert Maina, mfanyikazi wa hospitali ya kitaifa ya Kenyatta alikuwa akila mahaba na mpenziwe Joyce Maina Wangare wakati alipoteza fahamu na kukata roho. Ripoti ya polisi katika kituo cha Dandora ilionesha kwamba Wairimu aligutushwa na tukio hilo ambapo alikimbia kwenda kupiga ripoti.
CHANZO - TUKO NEWS
Social Plugin