Kwa mara ya kwanza msanii Harmonize amevunja ukimya kwa yanayoendelea mitandaoni kwa kusema atawafikisha Mahakamani wote ambao wanadaiwa kuvujisha picha, video na sauti siziso na maadili kwa lengo la kumchafua na kumdhalilisha.
Harmonize ametoa taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo kwanza amekana tuhuma hizo kwa kusema sio yeye kwenye picha na video hizo, pili atawafikisha Mahakamani wote waliohusika.
"Taarifa kwa Umaa, video zilizotengenezwa na kusambazwa mtandaoni zikiwa zinaonyesha sura yangu na kuunganishwa na utupu wa mtu mwingine kisha kuunganishwa na sauti yangu kwa lengo la kunichafua kunidhalilisha na kuharibu brand ambayo nimeitengeneza kwa mabilioni ya shilingi"
"Sitaki kujua aliyetengeneza ni nani au kaipataje ila ninachosema ni kwamba yeyote aliyehusika na hili suala linalolenga kunichafua na kunidhalilisha lazima watafikishwa mahakamani ili kukomesha chuki na tamaa zinazoathiri watu wasio kuwa na hatia, watanili?
Chanzo- Eatv
Social Plugin