Kulingana na Katibu wa kanisa la Virgin Mary Ordhodox James Warari alisema genge la wezi lilivamia kanisa hilo Alhamisi, Aprili 22,2021 na kuiba kengele hiyo ambayo inasemekana kuwa na uzito wa kilogramu 500.
"Kisa hicho kilitokea Alhamisi Usiku, tuliamka asubuhi na tukagundua kwamba kengele hiyo haikuwepo. Mtu mmoja hawezi akabeba kengele hiyo kwa sababu ni nzito sana. Tunajua kulikuwa na watu kadhaa walishirikiana kubeba," Warari alisema.
Warari alisema kengele hiyo ilikuwa imetengenezwa na shaba na ilikuwa ikitumiwa kuwakumbusha waumini saa za kuomba na pia kupanga ratiba ya kanisa hiyo.
Inasemekana kengele hiyo ilinunuliwa kutoka ng'ambo na Warari amemrai Mkenya yeyote ambaye atataka kuuziwa asiinunue bali awasiliane na wasimamizi wa kanisa hiyo.
"Tungependa mtu yeyote ambaye ataiona kengele hiyo awasiliane nasi, nisingependa inunuliwe na mtu yeyote, naomba ipelekwe afisi yoyote ya chifu ilioko eneo la Limuru, kengele hiyo ulinunuliwa ng'ambo na hatuwezi ipata nyingine kama hiyo hapa Kenya," Wariru alisema.
Social Plugin