Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BABA AGOMA KUZIKA MWILI WA MTOTO WAKE....ATAKA MWENYEKITI WA MTAA NA SUNGUSUNGU WAUFUFUE


Jeneza lenye mwili wa kijana Kusekwa George
***
Baba mzazi wa kijana Kusekwa George mkazi wa mtaa wa Ihushi kata ya Kishiri, Nyamagana Mwanza, amekataa kuhudhuria msiba na shughuli ya kuaga mwili wa mwanaye huyo mwenye miaka 17.

Mzee George amekataa akishinikiza mwili wa kijana huyo anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa na Mwenyekiti wa mtaa pamoja na Sungusungu, upelekwe kwa Mwenyekiti kisha amrejeshe mwanaye akiwa hai.

Kwa upande wa wakazi wa mtaa wa Ihushi kata ya kishiri wilayani Nyamagana mkoani Mwanza wamesema hawatauzika mwili wa kijana Kusekwa George.

Wananchi wamedai kuwa kijana huyo aliuawa kwa kupigwa na marungu, fimbo pamoja na mkanda wa mashine na mwenyekiti wa mtaa akishirikiana na Sungusungu.

Wananchi hao Aprili 8, 2021, wameupeleka mwili wa kijana Kusekwa nyumbani kwa Mwenyekiti huyo ili amrudishie uhai wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com