Wachimbaji wanne katika mgodi wa dhahabu wa Namba Mbili uliopo kijiji cha Ilujamate Wilaya ya Busega Mkoa wa Simiyu wamefariki dunia baada ya kufukiwa na vifusi baada ya kuta za duara kuporomoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Tukio hilo limetokea Aprili 12,2021 saa 4:25 usiku katika duara namba 18 na 17 AB na kusababisha vifo vya wachimbaji wanne na mwingine mmoja kujeruhiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Richard Abwao amesema aliyejeruhiwa ni Mangu Ngumba (33) mkazi wa Matongo Wilaya ya Bariadi na waliopoteza maisha ni Limbu Kisabo (28) mkazi wa Mwakibuga Wilaya ya Bariadi na Tembo Male (42) mkazi wa Isanga Bariadi.
Wengine ni Benjamini Masaka (51) mkazi wa Katoro Geita na Musa Washa (37) mkazi wa Dutwa Bariadi.
Via Mwananchi
Social Plugin