Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Video : RPC MAGILIGIMBA AIBUKIA KWENYE MABASI ALFAJIRI...AONYA MADEREVA WANAOKIUKA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba leo Jumapili Aprili 25,2021 saa 11 alfajiri amefanya ukaguzi wa kushtukiza kwa mabasi yaendayo mikoani kutoka Kituo Cha Mabasi Kahama na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa abiria na madereva wa magari hayo.

Kamanda Magiligimba amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kuepuka ku over take hovyo, kuendesha kwa speed kali huku akiwataka abiria kutoa taarifa pindi wanapobaini mienendo mibaya ya madereva wanapoendesha vyombo vya moto.

TAZAMA VIDEO HAPA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com