WANANCHI WACHANGIA MADAWATI 336, SH. MILIONI 5.6 SHULE YA SEKONDARI SOLWA , DC MBONEKO APONGEZA


Muonekano wa madawati yaliyotolewa na wananchi kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya sekondari Solwa

Na Shinyanga Press Club Blog
Wananchi wa Kata ya Solwa wilayani Shinyanga wameamua kutengeneza madawati 336 na kuyakabidhi katika shule ya Sekondari Solwa iliyokuwa na changamoto kubwa ya upungufu wa madawati kwa lengo la kutatua kero hiyo ambayo imekuwa ikisababisha wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini.

Mbali na msaada huo wa madawati, Wananchi hao wamechangia zaidi ya Sh. 5,600,000 kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo ili kupunguaza uhaba uliopo kwa sasa.

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na Shinyanga Press Club Blog wakati wakikabidhi madawati hayo wazazi hao waliotengeneza madawati zaidi ya 336 kwa gharama ya shilingi 23,6000,000 ikiwa ni nguvu zao wenyewe, wamesema wameamua kufanya hivyo ili kutokomeza upungufu wa madawati uliokuwepo awali ukisababisha wanafunzi kusoma wakiwa wamekaa chini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje amesema halmashauri iko tayari kutoa fedha za kukamilisha maabara ya shule hiyo, huku akimtaka Kaimu Mkurugenzi kufikisha suwala hilo panapohusika ili fedha hizo ziandaliwe mapema na kutolewa ili wanafunzi wa masomo ya sayansi wafanye vizuri katika masomo yao.

Naye, Diwani wa Kata ya Solwa, Awadhi Abood amesema licha ya wananchi kutengeneza madawati hayo 363 kwa nguvu zao wenyewe na kuchangia Sh. Milioni 5.6 za ujenzi wa vyoo vya wanafunzi, lakini pia wameweka mpango kazi wa kujenga madarasa manne zaidi kwa nguvu zao wenyewe ambapo mchanga na mawe tayari wameshakusanya.

Mkuu wa shule ya Sekondari Solwa, Thomas Manembe amesema kuwa msaada huo wa madawati umeifanya shule kuwa na ziada ya madawati 61.

Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko ambaye pia ni Menyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani humo, amewapongeza wananchi hao kwa juhudi zao za kusaidia na kutatua matatizo yanaisibu jamii yao, ambapo ametoa agizo wanafunzi watoro katika shule zote za wilaya hiyo wafuatiliwe na kurudi shuleni maramoja.

Vilevile, Mboneko ametoa onyo kwa baadhi ya wazazi wenye tabia ya kuwatupia mapepo wanafunzi haswa wasichana kwa lengo la kuwasababishia kufanya vibaya katika mitihani yao ya kuhitimu wakiwa na malengo kuwaozesha na kujipatia mali.

DC Mboneko pia amewataka wanafunzi wa shule hiyo kutumia nafasi ya elimu kutimiza malengo na ndoto zao kwa kuacha tamaa za kimwili zinazosababishwa na watu wasio na malengo mazuri juu yao.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kushoto) na baadhi ya viongozi mbalimbali wa kata ya Solwa wakiwa wameshikilia kiti ambacho ni sehemu ya msaada uliotolewa na wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kulia) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Ngasa Mboje (kushoto) wakiwa wameshikilia dawati ambalo ni sehemu ya msaada wa madawati 336 yaliyotolewa na wananchi kwa ajili ya shule ya Sekondari Solwa
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko (kushoto) na baadhi ya viongozi mbalimbali wa kata ya Solwa wakiwa wameshikilia kiti ambacho ni sehemu ya msaada uliotolewa na wananchi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje (kushoto) akimkabidhi msaada wa madawati, Mkuu wa Shule ya Sekondari Solwa, Thomas Manembe (kulia)
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akifurahia jambo na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Solwa baada ya kukabidhi msaada wa madawati uliotolewa na wananchi wa kata ya Solwa
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza shuleni hapo baada ya kukabidhi msaada huo uliotolewa na wananchi wa Kata ya Solwa

Sehemu ya madawati 336 yaliyotolewa na wananchi wa kata ya Solwa kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Solwa
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Ngasa Mboje akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi msaada huo
Diwani wa Kata ya Solwa, Awadhi Abood akizungumza wakati za zoezi la kukabidhi msaada huo shuleni hapo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Solwa akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa madawati 336 kutoka kwa wananchi, msaada ambao umeiwezesha shule hiyo kumaliza tatizo la madawati na kuwa na akiba ya madawati 61

 CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post