Mahakama ya Mwanzo Buguruni jijini Dar es salaam imevunja ndoa ya mwanamuziki wa nyimbo za injili, Rebecca Magaba na Zabron Maselege baada ya wanandoa hao kutoshiriki tendo la ndoa kwa zaidi ya miaka 18.
Mahakama hiyo imetoa amri mali zote walizochuma wanandoa hao, ikiwamo shamba la eka 10 lililopo Bagamoyo, maduka mawili yaliyopo Bonyokwa na Mahengo na shamba la miti ya mikaratusi lililopo Kigoma zichukuliwe na Maselege na kiwanja kilichopo Madale kitabaki kwa Rebecca.
Hakimu Mkazi, Mwinyiheri Kondo amesema Mahakama imevunja ndoa hiyo baada ya kuona wanandoa hao wanafanya matendo ya ndoa ambayo si ya kawaida.
Kondo amesema katika ushahidi uliotolewa na Rebecca alidai hawakuwahi kufanya tendo la ndoa tangu wafunge ndoa kutokana na mume wake kutokuwa na korodani.
Hivyo kutokana na hilo, Mahakama hiyo imevunja ndoa hiyo, na ndani ya siku 45 haki ya kukata rufaa kwa mdaiwa ipo wazi.
Katika kesi hiyo, Rebecca aliiomba Mahakama hiyo ivunje ndoa hiyo kisheria baada ya kuishi na mume wake kwa miaka 21 bila ya kushiriki tendo la ndoa.
Social Plugin