Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MHUBIRI ROBERT BURALE ASEMA MAPENZI HAYACHAGUI UMRI...WATU WAPENDANE


Tunafahamu watu maarufu kadhaa wameoana au kuolewa na wapenzi wanaowazidi kwa umri, mwanamuziki Bahati, Emmy Kosgei na Guardian Angel ni miongoni mwao.

Mashabiki mitandaoni wamekuwa wakiwashambulia, kuwatusi na kuwakashifu kwa kuoa wapenzi wakubwa kwa umri.

Mtaalamu wa Mapenzi Mhubiri Robert Burale kwa kauli yake amehoji kwamba hakuna mtu yeyote anastahili kutusiwa wala kukashfiwa kwa kuwa na mpenzi anayemzidi kwa umri mradi ana miaka 18.

 Burale amekuwa mstari wa mbele kuwatetea watu maarufu ambao wamekuwa wakikejeliwa na kukosolewa mitandaoni kwa ajili ya kuwa uhusiana wa kimapenzi na watu wa umri mkubwa. 

 Burale ambaye ni baba wa mtoto mmoja alisema kila mtu anapaswa kuishi maisha anayotaka, wale wanaochambua maisha ya wengine wanapaswa kujipatia shughuli.

 " Watu wawili ambao wamekomaa kiakili wakiamua kuoana, hakuna haja ya mtu kupinga uamuzi wao wala kukejeli na kuwakashifu hasa kama mmoja anamzidi mwingine kwa umri, kama hivyo ndivyo wanafurahia maisha na iwe hivyo." Alisema Burale.

 " Ni jambo la kukera sana kuona watu wakiingilia maisha ya wengine, kila mtu anafaa kuishi maisha yake," Aliongeza Burale. 

Kwenye taarifa ambazo zinahusiana na hii, mwanamuziki Emmy Kosgei amekuwa akikejeliwa sana kwa kuolewa na mwanaume ambaye anamshinda mara dufu kwa miaka. 

Emmy alisema alifanya uamuzi huo kwa sababu mumewe anaheshimu muziki wake, marafiki , mashabiki wake na kila mara yeye humsaidia katika kila hali anapokwama.

CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com