Na Kadama
Malunde – Malunde 1 blog
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Daud Lubambula (49) mkazi wa kijiji cha Kidana kata ya Ushetu wilayani Kahama ameuawa kwa kupigwa na chupa kichwani na kwenye mkono wa kulia na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikindika kata ya Kidana Andrew Adam.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora
Magiligimba amesema tukio hilo limetoa Aprili 18,2021 majira ya saa nne
usiku katika kitongoji cha Ikindika, kijiji cha Kidana, kata ya
Ushetu,tarafa ya Dakama, wilaya ya kipolisi Ushetu na mkoa wa Shinyanga.
“Daud
Lubambula aliuawa kwa kupigwa na chupa kichwani na kwenye mkono wa kulia
na mtuhumiwa huyo Andrew Adamu, hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi na
kupoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika kituo cha afya Ushetu”,amesema
Kamanda Magiligimba.
Amesema
chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi
uliotokana na ulevi kati ya marehemu na mtuhumiwa wakiwa kwenye kilabu cha pombe za kienyeji.
Ameeleza
kuwa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linatamfuta mtuhumiwa Andrew Adamu ambaye ni Mwenyekiti wa kitongoji cha Ikindika,
mkazi wa kitongoji cha Ikindika kwa kosa la mauaji.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga anatoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi
hilo ili kufanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Social Plugin