MBOWE ATEMA NYONGO TOZO ZA KODI....ASIMULIA ALIVYOKIMBIA NCHINI


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe ametaja sababu ya kuamua kuondoka nchini na kwenda kuwekeza nchi zingine kuwa ni tozo ya kodi kiasi cha Sh2 bilioni aliyopewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mbowe ameyasema hayo leo Jumapili Aprili 11, 2021 wakati akilihutubia Taifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, akidai kuwa kabla ya kupewa tozo hiyo aliondolewa dhamana katika kesi yake ya uchaguzi na kuwekwa ndani miezi minne na kipindi hicho TRA walimtumia barua pepe kuelezea deni hilo la kodi wakijua fika hakuwa katika nafasi ya kupata ujumbe huo.

“TRA ilisema ninadaiwa kodi ya takribani bilioni mbili kitu ambacho si kweli hakuna deni hilo. Unapoidai kampuni kodi hiyo ina maana inatengeneza faida kwa mwaka bilioni 12 kwa hiyo faida yake itakuwa bilioni 50, hii ni kampuni yangu ndogo ya kifamilia haiwezi kutengeneza hiyo fedha hata kwa miaka 20,” amesema Mbowe.
Chanzo- Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post