Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BINTI WA MIAKA 10 ABAKWA KISHA KUUAWA BAADA YA KUAGIZWA DUKANI


Binti mmoja mwenye umri wa miaka kumi mkazi wa Mtaa wa Rwazi Kata ya Kahororo, Bukoba amekutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa ambapo taarifa za madaktari zimeeleza kuwa alibakwa na kisha kuuawa.

Baba mzazi wa msichana huyo, Revocatus John, amesema binti yake alikutwa na mkasa huo baada ya kuagizwa dukani.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus Kinawilo, amefika nyumbani kwa wazazi wa marehemu kutoa pole sanjari na maagizo ya serikali.

"Mazingira ya kifo chake ni binadamu asilimia mia na ni uhalifu kwahiyo nimeliagiza Jeshi la Polisi liendelee kufuatilia nani alifanya hicho kitendo na katika hili wahuni wote kamata tutajuana kule kule Polisi" amesema Deodatus Kinawilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com