Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

IDDI NADO ASALIA AZAM FC MIAKA MIWILI TENA


Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
**
Kufuatia  kuonesha kiwango bora ndani ya Azam Fc Kiungo mshambuliaji wa wa timu hiyo Idd Seleman 'Nado', ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia kwa matajiri wa Chamazi.

Nado amesaini mkataba huo leo mchana mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', utakaomfanya aendelee kusalia Azam FC hadi mwaka 2024.

Popat amesema, Nado amekuwa na kiwango bora tokea msimu uliopita alipojiunga nao akitokea timu ya Jiji la Mbeya Mbeya City alipoonesha kiwango kikubwa hadi kuvutiwa naye.

Amesema, katika msimu wa 2020/21 Nado amehusika kwenye mabao 12 ya Azam FC, akifunga mara saba na kutoa pasi za mwisho tano.

Kwa sasa Azam Fc ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi akiwa na alama 47 nyuma ya vinara Yanga wenye alama 51 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu kwa alama 46.

CHANZO - MICHUZI BLOG


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com