Mfano wa panga likiwa kwenye moto
***
Mkazi wa Kata ya Marangu Mashariki wilayani Moshi, Baltazari Mtui anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuwaunguza makalio kwa kutumia panga la moto watoto wake wawili wa kiume.
Inadaiwa kuwa baba huyo aliweka panga kwenye moto kisha akawaunguza watoto hao ambao ni wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili katika Shule ya Msingi Lyasongoro.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Amon Kakwale alithibitisha kutokea tukio hilo Aprili 16, mwaka huu.
Via Mwananchi
Social Plugin