Mwenyekiti wa CCM, Mhe. Samia Suluhu Hassan
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi kumchagua kwa kishindo Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Sita wa CCM kwa kupata kura 1862, hakuna kura ya Hapana hivyo ameshinda kwa asilimia 100.
Rais Samia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye pia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kura zilizopigwa ni 1,862 ambapo kura za Ndiyo zilikua zote 1,862 ikiwa ni asilimia 100 ya kura zote.
Mara baada ya kutangazwa mshindi, Umoja wa Wanawake wa CCM wamemtunukia tuzo Mwenyekiti mpya wa CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan Mwenyekiti wa UWT, Gaudencia Kabaka amesema ushindi wa Samia unadhihirisha kuwa mfumo dume unaanza kutokomezwa kwenye nafasi za juu za uongozi kuanzia kwenye chama hadi serikalini.
Nafasi ya MNEC walioshinda ni Happiness Mgongo na Rehema Simba.
Social Plugin