MABINGWA watetezi, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Kagera Sugar mabao 2-0 jioni ya leo katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mabao ya Simba SC inayofundishwa na kocha Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa yamefungwa na kiungo wa kimataifa wa Msumbiji, Luis Miquissone dakika ya 13 na mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mugalu dakika ya 24.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 55 baada ya kucheza mechi 23, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na watani wao, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi.
Social Plugin