Mkurugenzi wa TANLAP, Christina Kamili akitoa neno la ufunguzi kwenye mafunzo hayo.
***
Mtandao wa Mashirika yanayotoa Huduma ya Msaada wa Kisheria Tanzania (TANLAP) umetoa mafunzo kwa waandishi wa Habari Mkoa Mwanza kuhusiana na Sheria na Kanuni zinazosimamia taaluma ya Habari ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari, Sheria ya Haki ya kupata Taarifa pamoja na Sheria ya Makosa ya Mtandao.
Mkurugenzi wa TANLAP, Christina Kamili amesema mafunzo hayo yaliyofanyika Aprili 28, 2021 jijini Mwanza yanalenga kuwajengea uelewa waandishi wa habari kutambua Sheria hizo na changamoto zake hatua itakayowasaidia kutimiza majukumu yao kwa weledi.
Alisema kupitia mafunzo hayo, pia waandishi wa habari watatambua wajibu wao wa kuibua migogoro na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo masuala ya mirathi ambao pia wanahitaji msaada wa kisheria.
“TANLAP kwa kushirikiana na wadau wengine tunasaidia wananchi kupata msaada wa kisheria bure hivyo kupitia mafunzo haya mtasaidia kuwaelimisha ili watambue taasisi zinazoweza kuwasaidia kupata haki zao mahakamani badala ya kujiwakilisha wenyewe kwa kukosa msaada” alieleza Kamili.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC), Edwin Soko alisema mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia weledi bila kuingia kwenye mvutano na Sheria zilizopo.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Wakili James Marenga alisema waandishi wa habari wanapaswa kuhakikisha hawaingii kwenye mgogoro na Sheria zinazoongoza taaluma yao na kuwahimiza kuzingatia sheria hizo ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari inayowataka kuwa na taaluma ya habari angalau kuanzia Stashahada.
Mafunzo hayo yametolewa na TANLAP kwa kushirikiana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) ikiwa ni sehemu ya kuelekea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yatakayofanyika Mei 03, 2021 yakiwa na kauli mbiu isemayo “Habari kwa Manufaa ya Umma”.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa TANLAP, Christina Kamili akifungua mafunzo hayo ambapo amesisitiza waandishi wa habari kuwaelimisha wananchi kutambua taasisi zinazotoa huduma ya msaada wa kisheria ili ziwasaidia kuoata haki.
Mkurugenzi wa TANLAP, Christina Kamili amesema Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria inataka makundi mbalimbali ya wananchi ikiwemo wenye ulemavu, wanawake na watoto kupata msaada wa kisheria bure kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Baadhi ya waandishi wa habari (kushoto) awakimsikiliza Mkurugenzi wa TANLAP, Christina Kamili wakati akifungua mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yamefanyika Monarch Hotel jijini Mwanza.
Meneja Programu TANLAP, Mchereli Machumbana akieleza umuhimu wa mafunzo hayo kwa Waandishi wa Habari.
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akizunguma wakati wa mafunzo hayo.
Wakili James Marenga akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada kutoka kwa Mwezeshaji, Wakili James Marenga.
SOMA>>> Habari zaidi hapa
Social Plugin