Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wa wilaya ya Bukombe yaliyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa
wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba ameeleza kufurahishwa na
mafunzo yanayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa wasindikaji,
wajasiriamali na wadau wa mchele kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya
viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi
zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Mhe. Nkumba
ametoa pongezi hizo leo Jumatano Aprili 28,2021 wakati akifungua mafunzo hayo
yaliyokutanisha wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele takribani 100 wa
wilaya ya Bukombe.
Amesema
mafunzo hayo ni njia muafaka ya kuleta tija zaidi katika juhudi za kuliletea
taifa maendeleo ya haraka kulingana na fursa zilizopo hasa kwenye sekta ya
viwanda,kilimo,biashara na maeneo mengine.
Ameongeza
pia Mafunzo haya ni uthibitisho wa azma ya Serikali kupitia taasisi zake katika
kufanikisha malengo ya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
Kwa upande
wake, Katibu Tawala wilaya ya Bukombe, Bw. Paul Cheyo amewataka wadau wa mchele
kutumia fursa ya mafunzo hayo kuongeza utaalamu katika uzalishaji na kuweza
kuthibitisha ubora wa bidhaa.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Bw. Dionis Myinga
amesema wadau wa mchele wanachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa nchi
hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kuzalisha bidhaa zilizokidhi viwango vya ubora
na usalama.
Meneja wa
Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala
amesema TBS inaendelea kutoa elimu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini
ili kuhakikisha kuwa wanapata elimu kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa
ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi
zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio ili kuleta ushindani na kukuza uchumi wa
nchi.
Mafunzo hayo
yameandaliwa na TBS na yamefanyika katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na
yataendelea kwenye wilaya ya Katoro mkoani Geita na kumalizika katika wilaya ya
Sengerema mkoani Mwanza.
Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba akizungumza leo Aprili 28, 2021 wakati akifungua mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wa wilaya ya Bukombe yaliyotolewa na TBS kwa ajili kutoa elimu kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba akizungumza wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na TBS kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Mkuu wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita Mhe. Said Nkumba akiishukuru na kuipongeza TBS kuendesha mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio. Kulia ni Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala, katikati ni
Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala akielezea lengo la TBS kutoa elimu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini ambapo amesema ni kuhakikisha kuwa wanapata elimu kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio. Kushoto ni Katibu Tawala wilaya ya Bukombe, Bw. Paul Cheyo.
Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Joseph Ismail Mwaipaja akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Bw. Dionis Myinga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Bw. Dionis Myinga akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Katibu Tawala wilaya ya Bukombe, Bw. Paul Cheyo akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw. Hamisi Sudi Mwanasala akizungumza wakati wa mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo yaliyotolewa na TBS kuhusu kanuni bora za uzalishaji, matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Soma pia
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com