Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AKAUNTI ZA BENKI ZA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU 'THRDC' ZAFUNGULIWA


Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umesema akaunti za benki za mtandao zilizofungwa kwa takribani miezi minane zimefunguliwa.

THRDC imetoa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake unaojali na kuzingatia haki za binadamu na utawala bora.

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatano Aprili 21, 2021 na bodi ya mtandao huo na kutoa shukrani kwa wahisani, taasisi mbalimbali na wanachama walioshiriki kwa namna mbalimbali kuhakikisha mtandao unaendelea kutekeleza majukumu yake pia kuhakikisha kuwa changamoto husika zinatatuliwa.

Taarifa hili imeeleza kuwa kufunguliwa kwa akaunti hizo kumetokana na maelekezo kutoka kwa mamlaka za Serikali zilizoagiza kufungwa ili uchunguzi wa tuhuma ufanyike na kisha kutoa maelekezo kuwa zifunguliwe.

Via MWANANCHI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com