Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. EDWARD HOSEAH ACHAGULIWA KUWA RAIS WA TLS


Dkt. Edward Hoseah
***
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimefanya uchaguzi wa Rais ambapo Dkt. Edward Hoseah ameibuka mshindi wa nafasi hiyo kwa kupata kura 297 katika uchaguzi uliojaa ushindani mkali.

Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Aprili 16, 2021 Jijini Arusha, mshindani wa karibu wa Dk. Hoseah Flaviana Charles amepata kura 223.

Dk. Hoseah amewahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dk. John Magufuli kutengua uteuzi wake mwaka 2015.

Kwa ushindi huo Dk. Edward Hoseah sasa anachukua nafasi ya Rais wa TLS anayemaliza muda wake Dk. Rugemeleza Nshala ambaye naye alichukua kijiti cha kuiongoza TLS kutoka kwa mtangulizi wake Fatma Karume.

 Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com