Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vifaa vya kupigia ramli chonganishi Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanya Operesheni maalumu ya kukabiliana na kuzuia
makosa ya uhalifu na kufanikiwa kukamata wahalifu 231 wanaojihusisha na unyang’anyi
wa kutumia silaha, wakata mapanga na waganga wa jadi wanaojihusisha na upigaji
ramli chonganishi ambazo ni chanzo na kichocheo cha mauaji ya imani za
kishirikina.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamisi Aprili 29,2021, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema Operesheni hiyo imefanyika
kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021 ambapo jumla ya watuhumiwa 231
walikamatwa,kati yao wanawake ni 71 na wanaume 160.
“Watuhumiwa
169 kati ya 231 wamefikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria na
watuhumiwa 62 waliobaki watafikishwa mahakamani baada ya upelelezo kukamilika”,ameeleza
Kamanda Magiligimba.
“Katika
Operesheni hiyo tulifanikiwa kukamata Bunduki 14 kati ya hizo gobore 13 na
Shortgun moja ilitengenezwa kienyeji. Bangi kilogramu 65 na mashamba ya bangi
ekari 6,madawa ya kulevya aina ya
Heroine gramu 300,mirungi kilogramu 3 na gramu 250”,ameeleza.
Amesema pia
walikamata magari mawili yenye namba za usajili T.673 AYK Toyota Sprinter na
T.377 DNA Toyota IST, pikipiki 19 aina ya
SANLG, mazao ya misitu mbao 711 na pombe ya Moshi lita 407 pamoja na
mitambo mine ya kutengenezea pombe ya kienyeji (moshi).
Mali zingine
zilizokamatwa ni boksi 30 za Kondomu zilizopigwa marufuku, TV 14, Radio Sabufa
6, Computer 3, magodoro 12, mabati 15, betri za magari 12, baiskeli,jiko la gesi, betri za pikipiki 6,
betri za solar 7, simu 7,mafuta ya diesel lita 240,Engine Oil lita 120,vitenge
pc 42 pamoja na magauni 15 ya vitenge, maturubai mawili ya magari makubwa,
nondo 36 na mabomba matano ya maji.
Kamanda
Magiligimba ameongeza kuwa Operesheni hiyo pia ilinasa bidhaa mbalimbali
zilizokwisha muda wake na madawa mbalimbali,vifaa tiba, vifaa mbalimbali vya
kufanyia uhalifu,noti bandia 7 kati ya hizo 6 ni za elfu 5, moja elfu 10,
mifuko ya nailoni iliyopigwa marufuku 1200 na mawe yadhaniwayo kuwa na dhahabu
kilogramu 2.
Amesema
misako hiyo ni endelevu ikiwa ni pamoja
na kubaini mitandao yote ya kihalifu ili kukabiliana nayo huku akiwasisitiza
wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu kwa jeshi la polisi na
kwamba kamwe jeshi la polisi halitasita kuchukua hatua kali kwa mtu yeyote
anayejihusisha na matukio ya uhalifu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu Operesheni Maalumu iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021 ambapo jumla ya watuhumiwa 231 walikamatwa,kati yao wanawake ni 71 na wanaume 160. Picha na Kadama Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha bunduki zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha bangi zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha mabati yaliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha pikipiki zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha baiskeli iliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vifaa vya kupigia ramli chonganishi vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vifaa vya kupigia ramli chonganishi vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha baiskeli iliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha moja ya TV zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha bangi zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha magodoro yaliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha moja ya jiko la gesi lililokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha pombe ya kienyeji/moshi iliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vipodozi vilivyokwisha muda wake vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vifaa vya kuzimia moto vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha mashine iliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha panga la kufanyia uhalifu lililokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha kahawa iliyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Muonekano wa vipodozi vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Muonekano wa pombe za kienyeji na vifaa tiba vilivyokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Mali mbalimbali zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,2021
Sehemu ya pikipiki zilizokamatwa wakati wa Operesheni Maalumu ya kukabiliana na kuzuia makosa ya uhalifu mkoani Shinyanga iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga kuanzia Mwezi Januari 2021 hadi Aprili 25,202.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com