Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Ummy Mwalimu amemsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Magesa Boniphace kuanzia leo 20 Aprili, 2021 ili kupisha uchunguzi dhidi yake.
Amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi na viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo, Hamis Tabasamu kuhusu tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo.
Tuhuma hizo zinasema Mkurugenzi kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara, wamekuwa wakifanya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za Umma zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Social Plugin