TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Bwana amesema, katika
Mkutano huu Tume imetoa uamuzi wa Rufaa 151
na Malalamiko 11 yaliyowasilishwa na
watumishi mbalimbali wa umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na
Mamlaka zao za Ajira na Mamlaka za Nidhamu.
Kati ya rufaa 151
zilizotolewa uamuzi na Tume rufaa 82
zimekataliwa; rufaa 43 zimekataliwa
kwa kuwa ziliwasilishwa nje ya muda uliowekwa kwa mujibu wa Sheria. Rufaa 12 zimekubaliwa; rufaa 11 zimekubaliwa kwa masharti kwamba
zikashughulikiwe upya na Mamlaka zao za Nidhamu kwa kuzingatia Sheria, Kanuni
na Taratibu. Rufaa 3 hazikutolewa
uamuzi kwa sababu ni kesi zilizopo
Mahakamani.
Kwa upande wa malalamiko, Tume ilipokea na kutoa
uamuzi wa malalamiko 11 ambapo
malalamiko 6 yamekataliwa,
malalamiko 4 yamekubaliwa na lalamiko
1 limekataliwa kwa sababu
liliwasilishwa nje ya muda.
Imeandaliwa na:-
Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini
Tume ya Utumishi wa
Umma
DAR ES SALAAM
23 Aprili, 2021
Social Plugin