ZITTO KABWE AICHAMBUA RIPOTI YA CAG



Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amechambua na kuainisha maendeo 10 katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), huku akiitaka Serikali kufanya uchunguzi wa kina kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Zitto amefanya uchambuzi huo leo Jumpili, Aprili 11, 2021 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam ambapo pia amegusia makusanyo ya kodi yapo chini, huku akitaka fedha zote zilizochukuliwa na DPP kutokana na kesi za mbalimbali zirejeshwe.

Pia amegusia madai ya wazabuni dhidi ya Serikali yaliyofikia Sh3.1trilioni, huku akisema Sh2.2 trilioni hazikupita Mfuko Mkuu wa Hazina na Hivyo kutoidhinishwa na CAG matumizi yake.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post