Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara zenye dhamana yaElimu,Michezo na TAMISEMI wakiwa kwenye kikao kazi leo Aprili 27,2021 Jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana hizo hizo kwa lengo la kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uimarishaji wa somo la Elimu kwa Michezo na Michezo katika shule za Msingi na Sekondari hapa nchini chini ya uenyekiti wa Prof.Riziki Shemdoe ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI.
Dkt. Hasssan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia eneo la Elimu ndugu Gerard Mweli (kulia) wakihudhuria kikao cha Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara zenye dhamana ya Elimu, Michezo na TAMISEMI wamefanya kikao kazi leoAprili 27,2021Jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana hizo hizo kwa lengo la kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa masuala mbalimbali yauimarishaji wa somo la Elimu kwa Michezo na Michezo katika shule za Msingi na Sekondari hapa nchini. Upande wa pili ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusufu Omary Singo
Na John Mapepele, Dodoma
Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara zenye dhamana ya Elimu, Michezo na TAMISEMI wamefanya kikao kazi leo Aprili 27,2021 Jijini Dodoma kujadili utekelezaji wa maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana hizo hizo kwa lengo la kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uimarishaji wa somo la Elimu kwa Michezo na Michezo katika shule za Msingi na Sekondari hapa nchini
Mwenyekiti wa Kikao hicho, Prof. Riziki Shemdoe ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI amesema miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa na kukamilika ni pamoja na kuandaliwa kwa mapendekezo ya uimarishaji wa ufundishaji wa somo la michezo shuleni na tahasusi zenye somo hilo kwa kidato cha tano ambapo ameseme tahasusi hizo zitaanza kufundishwa katika mwaka huu wa masomo.
Pia rasimu ya Mpango Mkakati na Mikakati ya utekelezaji wa masuala mbalimbali ya somo la Elimu kwa michezo na michezo katika shule za Msingi na Sekondari imeandaliwa ili kuboresha michezo mashuleni.
Kuhusu kuandaa kiunzi cha uendeshaji wa michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA Prof. Shemdoe amesema tayari Kamati ya Wataalam imeshauri kuwa kwa sasa miongozo iliyopo itumike na kiunzi tayari kimeshaandaliwa kwa kuzingatia changamoto zilizopo ambapo kitajadiliwa na wadau wote Juni mwaka huu wakati wa michezo ya UMISHUMTA NA UMISSETA na kwa sasa tayari miongozo hiyo imeshatumwa kwenye mikoa yote hapa nchini.
Aidha, suala la uundwaji wa Kamati ya kitaifa ya UMISHUMTA NA UMISSETA tayari imependekezwa na kukubalika kuundwa kwa Kamati ya Usimamizi itakayoundwa na wataalam wawili wawili kutoka kwenye kila Wizara ambapo imekubalika kuwa pamoja na usimamizi, Kamati itatumia fursa hiyo kujifunza na kuangalia changamoto zilizopo kwenye uendeshaji wa michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA kuandaa mapendekezo yatakayojadiliwa na wadau wote kwa ajili ya maboresho zaidi.
Prof. Shemdoe amesema kuhusu mchakato wa maandalizi ya UMISHUMTA NA UMISSETA mwaka huu, tayari mikoa yote imeshaandikiwa barua ya taarifa na Mhe. Waziri Ofisi ya Rais –TAMISEMI na kwamba waratibu wa michezo wanakwenda kwenye ukaguzi wa viwanja na maeneo ya malazi na chakula kuanzia Aprili 28-30, mwaka huu. Pia Kamati ya wataalam inaendelea na ufuatiliaji wa Shule teule za michezo ili kuhakikisha kuwa michezo inafanyika kwenye kiwango kinachotakiwa.
Makatibu Wakuu walioshiriki kwenye kikao hiki ni pamoja Mwenyekiti wa kikao hicho, Prof. Riziki Shemdoe ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI,na Naibu wake anayeshughulikia eneo la Elimu ndugu Gerard Mweli, mwingine ni Dkt. Hasssan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Dkt. Leonard Akwilapo kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojioa pamoja na Watendaji mbalimbali kutoka Wizara hizo.
Maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana ya elimu, Michezo na TAMISEMI yalitolewa wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika Februari 8, Mwaka huu.