Mchoraji mmoja kutoka Misri amepata mashabiki wengi katika taifa hilo la Afrika Kaskazini hasa wapenzi wa soka wanaovutiwa na mchezo wa Nyota wa Barcelona Lionel Messi.
Hii ni kwa sababu ya jamaa huyo Islam Mohammed Ibrahim Battah mwenye umri wa miaka 27 kufanana sana na nyota huyo raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 33 anayeichezea klabu ya Barcelona .
''Nilipoanza kuacha ndevu zangu rafiki zangu waliniambia nilikuwa nafanana na Messi . Nilipoacha zikawa ndefu hata zaidi nilifanana naye hata kabisa'' Aliliambia shirika la Habari la Reuters .
Katika ziara mjini Zagazig kilomita 90 kaskazini mwa mji mkuu Cairo watoto katika hifadhi inayowapa malezi walifurahi sana .
Akiwa amevalia jezi ya Barcelona Battah alicheza soka na watoto hao kwenye uwanja wa mazoezi ulio karibu ,shirika la Reauters lina furaha ya watoto hao kuona jinsi Battah anavyofanana na Messi kwa kutoweza kutofautisha ni kitu 'kisichoweza kuelezeka'.
" Ukimfanya mtu afurahi ,Mungu anakuwazadi.Nilitaka wawe na furaha hii nami''
CHANZO - BBC SWAHILI
Social Plugin