Mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari Kabugalo iliyopo Bukoba mkoani Kagera Gisera Oswardi (18) amefariki dunia kwa kupigwa na radi huku mwalimu wake akijeruhiwa.
Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea leo Alhamisi Aprili 15, 2021 saa tatu asubuhi ambapo mwanafunzi huyo akiwa na mwalimu wa shule hiyo Charles Alphonce walipigwa na radi wakati wanatoka darasani kwenda ofisini.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera Dkt. Mselata Nyakiroto amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kifo cha mwanafunzi huyo kimetokana na radi kumuunguza sehemu kubwa za mwili wake.
Social Plugin