Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHIREFA YATANGAZA VIINGILIO MWADUI VS SIMBA, YAWATAKA MASHABIKI KUJITOKEZA KWA WINGI

Mwenyekiti wa Shirefa, Said Mankiligo

Na Damian Masyenene, SHINYANGA 
CHAMA cha Soka Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) kimesema kuwa maandalizi yote ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) baina ya Mwadui FC NA Simba SC utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga yamekamilika.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa SHIREFA, Said Mankiligo, hali ya uwanja wa CCM Kambarage ni nzuri, maandalizi ya uuzaji tiketi yamekamilika, huku akibainisha kuwa wenyeji Mwadui FC wameahidi ushindi kwa Wana Shinyanga, hivyo akwaomba mashabiki wa timu zote mbili kujitokeza kwa wingi uwanjani hapo.

Mankiligo ameeleza kuwa viingilio vya mchezo huo vitakuwa Sh 5,000 kwa mzunguko na Sh 10,000 kwa jukwaa kuu (VIP), ambapo milango ya uwanja huo itafunguliwa saa 6 mchana na tiketi zitauzwa katika mageti manne.

“Maandalizi yote yamekamilika, hali ya uwanja ni nzuri, kazi kwa timu tu kuonyesha ufundi wao. Tayari timu zote zimeshawasili, tunawakaribisha mashabiki wote kufika kwa wingi kuzishuhudia timu zao.

“Kikubwa Zaidi, naomba timu zote mbili zituonyeshe burudani iliyo bora, wananchi wa Shinyanga wanayo hamu ya kuona burudani, tunaiombea Mwadui iweze kupata alama tatu na tunajua wamejiandaa kwa ajili ya hilo.

“Mwadui wametuahidi kwamba watakwenda kupambana kufa kupona na kuonyesha kwamba siyo timu ya kudharauliwa kama inavyoonekana. Na wameahidi kwamba watafufukia kwa Simba,”
amesema.




Picha zikionyesha maandalizi mbalimbali ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga utakaotumika kwa mchezo wa ligi kuu kati ya Mwadui FC na Simba SC kesho




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com