Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Na Kadama
Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa
mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga katika mnyororo wa thamani kuhusu
kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu
ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Mafunzo hayo
yamefanyika leo Jumanne Aprili 27,2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Kahama na kukutanisha wajasiriamali 100 wanaojihusisha na bidhaa ya Mchele
ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.
Akifungua mafunzo
hayo, Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha aliishukuru TBS kwa
kukutana na wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele akieleza kuwa ni
kundi la wajasiriamali ambao ni sehemu muhimu katika sekta binafsi inayochangia
pato la taifa,kuongeza ajira na kuondoa umaskini nchini.
“Wilaya ya Kahama ni moja ya wilaya za
kimkakati katika uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo, madini na biashara,
hivyo basi uzalishaji,uuzaji na usambazaji wa mchele ni sehemu ya shughuli kuu
kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wakubwa katika wilaya ya Kahama”,alisema
Macha.
Licha ya
kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia ubora,viwango na usalama pia
aliwakumbusha kuwa waaminifu kwa wateja wao kwa kuepuka kuchanganya mchele kutoka maeneo tofauti na
kuuza kwa bei juu.
Aidha
aliwasihi wafanyabiashara wa mchele kuwa wazalendo na kuepuka kushirikiana na
wafanyabiashara kutoka nje ya nchi wanaokuja na vifungashio vyao na
kutambulisha mchele wa Tanzania kuwa unazalishwa katika nchi hizo akibainisha
kuwa kitendo hicho ni kuhujumu uchumi wa nchi.
Kwa upande
wake, Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Hamisi
Sudi Mwanasala alisema TBS inataka bidhaa nzuri zifungwe kwenye vifungashio
sahihi zikiwa na taarifa sahihi ili kulinda afya za watumiaji.
Alisema TBS
inaendelea kutoa elimu kwa wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini ili
kuhakikisha kuwa wanapata elimu na utaalamu kuhusu kanuni bora za uzalishaji,
matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa
za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio ili kuleta ushindani na kukuza
uchumi wa nchi.
Mafunzo hayo
yameandaliwa na TBS kama moja ya utekelezaji wa makubaliano ya kikao cha wadau
katika mpaka wa Sirari ambacho kiliadhimia TBS kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wasindikaji
na wadau wa mchele katika Kanda ya Ziwa.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama leo Jumanne Aprili 27,2021. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akifungua Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakifuatilia mafunzo kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Hamisi Sudi Mwanasala akizungumza wakati wa Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa Joseph Ismail Mwaipaja akizungumza wakati wa Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Katibu wa Wamiliki wa Mashine za Kukoboa Mpunga Malunga, Mjini Kahama, Michael Nyahiti akizungumza wakati wa Mafunzo kwa wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Meneja wa Utafiti na Mafunzo Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Bw.Hamisi Sudi Mwanasala, Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa Joseph Ismail Mwaipaja na Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mashine za Kukoboa Mpunga Kagongwa wilayani Kahama (kulia) wakiwa ukumbini.
Kushoto ni Afisa Mdhibiti Ubora TBS, Evarist Mrema na Katibu wa Wamiliki wa Mashine za Kukoboa Mpunga Malunga, Mjini Kahama, Michael Nyahiti wakiwa ukumbini.
Afisa Udhibiti Ubora Mkuu TBS, Cunbert Kapilima akiwasilisha mada kuhusu ufungishaji na uhifadhi wa mchele
Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa, Joseph Ismail Mwaipaja akiwasilisha mada kuhusu TBS na majukumu yake
Afisa Masoko wa GS1 Tanzania, Shaban Mikongoti akiwasilisha mada kuhusu teknolojia ya usindikaji mchele
Afisa Afya wa Manispaa ya Kahama, Basil Gervas Kafunja akiwasilisha mada kuhusu kanuni bora za usafi na utunzaji wa mchele
Afisa Viwango wa TBS, Zena Issa akiwasilisha mada kuhusu utaratibu wa kuthibitisha ubora na faida za kutumia alama za ubora
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakifuatilia mafunzo kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini wakifuatilia mafunzo kuhusu kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango,namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Mafunzo yanaendelea

Maafisa kutoka TBS wakiandika dondoo muhimu kwenye mafunzo ya Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha na Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha, Wafanyakazi wa TBS na Wasindikaji, wajasiriamali na wadau wa mchele wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Soma pia
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com