Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa Bw.Ismail Joseph akitoa mada kwa washiriki wa Mafunzo kwa wadau wa bidhaa ya mchele yaliyofanyika Katoro wilayani Geita.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wadau wa mchele katika mji mdogo wa Katoro wilayani Geita wakifuatilia mafunzo.
Mafunzo haya yanalenga kutoa elimu kuhusu mnyororo wa thamani wa bidhaa ya mchele , kanuni bora za uzalishaji,matakwa ya viwango, namna bora ya uhifadhi,elimu juu ya vifungashio na taarifa za msingi zinazotakiwa kuwepo kwenye vifungashio.
Shirika la Viwango Tanzania [TBS] limetoa mafunzo kwa wadau wa mchele Mji mdogo wa Katoro wilaya ya Geita mkoani Geita.
Akitoa mafunzo hayo leo kwa washiriki, Meneja wa TBS Kanda ya ziwa Mhandisi Joseph Ismail Mwaipaja amewataka kuzingatia Viwango kabla ya kuzipeleka bidhaa zao sokoni.
Aidha Mhandisi Mwaipaja amewafundisha washiriki majukumu ya TBS ikiwa ni pamoja na kuwaeleza huduma zinazotolewa na namna gani wao kama wadau wanaweza wakafaidika na kuleta tija kwa biashara zao.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki waliopata mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yana tija kwao na yamekuja wakati muafaka hususani katika kipindi hiki cha msimu wa Mavuno ya mpunga huku wakiishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kupata mafunzo kwani yatawasaidia kuthibitisha ubora wa bidhaa zao na hatimaye kuuza mazao yao nje ya nchi.
Social Plugin