Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Kitila Mkumbo,akizungumza na viongozi pamoja na wafanyabiashara wa soko la Kariakoo la jijini Dar es saalam (hawapo pichani) wenye lengo la kusikiliza changamoto zilizopo katika soko hilo kilichofanyika leo April 13,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo Dar es salaam wakimsikiliza Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Kitila Mkumbo,wakati walipokutana naye na kufanya kikao chenye lengo la kusikiliza changamoto zilizopo katika soko hilo kilichofanyika leo April 13,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Kitila Mkumbo,akimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania Mchungaji Silver Kiondo,wakati akimuelezea changamoto zilizopo katika Soko la Kariakoo Dar es salaaam mara baada ya Waziri kukutana na viongozi pamoja na wafanyabiashara wa soko la Kariakoo la jijini Dar es saalam kikao chenye lengo la kusikiliza changamoto zilizopo katika soko hilo kilichofanyika leo April 13,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Kitila Mkumbo,akimsikiliza Katibu wa Jumuiya hiyo Bw. Abdallah Mwinyi wakati wa kikao cha viongozi na wafanyabiashara wa soko la Kariakoo jijini Dar es saalam chenye lengo la kusikiliza changamoto zilizopo katika soko hilo kilichofanyika leo April 13,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo Dar es Salaam wakifatilia kikao chao dhidi ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Prof.Kitila Mkumbo alipokutana nao kusikiliza changamoto pamoja na kero zilizopo katika soko hilo leo April 13,2021 Jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Kitila Mkumbo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi na wafanyabiashara wa soko la Kariakoo la jijini Dar es saalam kwa lengo la kusikiliza changamoto zilizopo katika soko hilo ili kuzitatua na kutengeneza mfumo mzuri kwa wafanyabiashara wa soko hilo.
Akizungumza na wafanyabishara hao Leo April 13,2021 jijini Dodoma baada ya kusikiliza changamoto zao Waziri Mkumbo amesema lengo la serikali ni kuona wafanyabiashara wanafanya biashara katika mazingira mazuri na kuchangia uchumi wa nchi.
“Lengo langu ni kutaka kuona Kariakoo ya zamani inarudi, kwa sababu soko hili ndio tunalitegemea katika kukusanya mapato na ili tukusanye mapato lazima wafanyabiashara wafanye biashara vizuri bila vikwazo wala manung’uniko” amesema Waziri Mkumbo.
Mara baada ya kusikia kero zinazowakumba wafanyabiashara hao amesema April 18, 2021 atafanya mkutano na kuwakutanisha wafanyabiashara, waagizaji wa bidhaa nje ya nchi, maafisa wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya bandari Tanzania (TPA),
“Nataka nikutane na ninyi wote kwa umoja wenu na mimi nitakuja na Waziri mwenzangu wa Fedha na Mipango, maafisa wa TRA, TPA ili changamoto zenu zijibiwe papo hapo, kama za kisera ziende Bunge na za utendaji zikafanyiwe kazi na ninataka mkutano ufanyike maeneo yaleyale ya Kariakoo” amesema.
Amesema na mambo yote watakayokubaliana yataingia katika utekelezaji na watakuwa wakifanya tathmini mara baada ya kipindi flani ili kuona kama yana manufaa kwa pande zote mbili lengo ni kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya biashara katika mazingira mazuri na kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.
Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania Mchungaji Silver Kiondo, amemwambia Waziri kuwa kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakifanya mazungumzo mara kwa mara lakini hakuna mabadiliko yoyote ya kiutendaji katika changamoto wanazokubaliana.
Amesema kuna haja ya Serikali kuipitia upya sera ya sheria ya kodi ya forodha kwani wao kama wafanyabiashara wanaona inachangamoto kwao katika kuitekeleza, mara nyingi wafanyabiashara wanachukua mizigo nchi za Kenya na Uganda, wakati wangeweza kutumia bandari ya Dar es saalam na serikali kupata mapato.
“tulikuwa tunaomba sera ya sheria za kodi zirudishwe Bungeni tunauhakika zitarudi zimebadilika kutoka zilivyo hivi sasa sisi tunaona sio rafiki kwetu kabisa, licha kuwa ni za jumuiya ya Afrika Mashariki lakini tunaomba zitazamwe upya” amesema Kiondo.
Aidha wameiomba Serikali inapofanya mabadiliko ya kodi au makadirio ya kodi kuwaarifu wafanyabiashara kwani mabadiliko yanayofanyika mara nyingi yanawapa wakati mgumu baadhi ya wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kwa oda ya mwaka mzima.
Nae Katibu wa Jumuiya hiyo Bw. Abdallah Mwinyi amesema mwanachama yeyote wa Jumuiya hiyo lazima awe mfanyabiashara na biashara inayotambulika, na wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi sana na wanaamini kama zitatatuliwa kutakuwa na mabadiliko makubwa katika ufanyaji biashara na ukusanyaji wa mapato.
Social Plugin