UKURASA WA HISTORIA WAGEUKA CUBA: RAUL CASTRO KUACHIA NGAZI


Katika siku chache, Fidel Castro hatakuwa tena madarakani nchini Cuba: kongamano la Chama cha Kikomunisti, ambalo lilifunguliwa jana Ijumaa, litasitisha miongo sita ya utawala wa kidugu ambao sasa unaachia kizazi kipya nafasi.

Baada ya kifo cha Fidel Castro mnamo mwaka 2016, kustaafu kwa Raul, ambaye hivi karibuni atatimiza umri wa miaka 90, ambaye alimkabidhi kijiti cha uongozi wa nchi Rais Miguel Diaz-Canel, 60, ukurasa wa kihistoria kwa kisiwa hicho na wakaazi wake unabadilika, ambapo karibu wakaazi wote wa Cuba hawaijui familia yoyote katika uongozi wa nchi hiyo kuliko ile ya wanamapinduzi maarufu.

"Raul hatakuwa kiongozi wa chama tena, lakini ikiwa kuna tatizo Raul atakuwepo, hajafa", Ramon Blande, mwanaharakati wa kikomunisti, 84, amesema.

Kuanzia  jana saa 3:00 asubuhi (sawa na saa7:00 mchana ), wajumbe zaidi ya mia moja wa chama kimoja, kutoka majimbo yote, watakutana kwa siku nne hadi siku ya Jumatatu  katika mji mkuu, kwenye vikao mbalimbali, kujadili maswala makubwa ya nchi.

Uteuzi wa Bwana Diaz-Canel kama katibu mpya wa kwanza, wadhifa muhimu zaidi nchini Cuba, unatarajiwa kufanyika siku ya mwisho, Jumatatu.

 

-RFI




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post