Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena akitoa taarifa ya kurejeshwa kwa vijana wa kujitolea katika mafunzo ya JKT kuanzia Mei 7 hadi 14, 2021 baada ya kuwarejesha nyumbani hapo awali.
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limewataka vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya kujitolea kuripoti katika makambi waliyopangiwa kati ya Mei 7 hadi 14, 2021 lakini utaratibu huo hautawahusu wenye elimu ya kidato cha sita, cheti, stashahada, shahada na taaluma ya uhandisi.
Kaimu mkuu wa utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan Mabena, amewaambia wanahabari kuwa vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi waliyopangiwa awali.
Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala (JKT), Kanali Hassan Mabena amesema, vijana hao wanatakiwa kuripoti katika kambi walizokuwa wamepangiwa awali kuanzia Mei 7 hadi Mei 14,2021.
“Vijana waliorejeshwa ni wale wenye elimu ya darasa la saba na kidato cha nne, wenye elimu ya kidato cha sita, ngazi ya cheti, stashahada, shahada na wale wenye Taaluma ya Uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa"', amesema Kanali Mabena
Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) limekuwa likiendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana kwa kuwapa stadi za maisha ikiwa ni pamoja na uzalishaji mali, uzalendo, kilimo, ufugaji na kushiriki katika ujenzi wa Taifa.
Mwezi Februari mwaka huu, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) alitangaza kuwarejesha nyumbani zaidi ya vijana 12,000 hadi ambapo wangetangaziwa tena.