Kiongozi wa akina mama katika kanisa hilo Mama Prisca Orembo amesema walipata habari kuhusu tukio hilo Jumapili, Aprili 18,2021.
“Tulifahamishwa kwamba kuna tukio kanisani na tulipofika hapo tulithibitisha ni kweli, wezi walivunja mlango wa kanisa na katika makazi ya mchungaji," Mama Prisca Orembo alinukuliwa na Citizen.
Duru zinaarifu kwamba wezi hao waliiba mali kadhaa ikiwemo nguo za ndani za pasta na chakula chake jikoni.
“Wezi hata wanaiba nguo za ndani za pasta wanaenda kuuza, hii ni nini?" alisema Wycliffe Sajida, ambaye ndiye pasta wa kanisa hilo.
Pasta huyo alisema alipoteza kila kitu wakati wa kisa hicho.
“Walichukua suti mbili, mashati matano, viatu, mtungi wa gesi, nguo za kuhubiri na KSh. 2,500,” pasta Wycliffe alisema.
Waumini wa kanisa hilo sasa wanataka idara ya polisi eneo hilo kuchukuwa hatua na kuwasaka wezi hao.
Social Plugin