Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WASHTAKIWA 243 WAKIRI MAKOSA, WALIPA FIDIA, FAINI BILIONI 35.07


WAZIRI wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema kiasi cha shilingi bilioni 35.07 kimepatikana baada ya washtakiwa mbalimbali kukiri kutenda makosa.

Profesa Kabudi amesema hayo Leo April 28, 2021 bungeni mjini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Amesema Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imeendelea kutekeleza zoezi la makubaliano ya kumaliza kesi za jinai chini ya utaratibu wa washtakiwa kukiri makosa yao kwa mujibu wa sheria ya marekebisho ya sheria namba 11 ya mwaka 2019.

Amesema katika kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021, kesi 192 zilihitimishwa kwa njia hiyo, na jumla ya washtakiwa 243 walikiri makosa na kulipa kiasi cha shilingi bilioni 35,07 kama fidia pamoja na faini kutokana na makosa ya uhujumu uchumi.

“Zoezi hili ni endelevu na fedha hizi zimewekwa katika akaunti maalum iliyoko Benki Kuu ya Tanzania,” amesema Profesa Kabudi




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com