Picha : BENKI YA CRDB YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA SHINYANGA

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi imetoa Futari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kutii maelekezo ya Dini ya Kiislamu yanayoelekeza umuhimu wa kufuturisha watu kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Akikabidhi Futari hiyo leo Jumamosi Mei 8,2021 Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Said Pamui amesema Benki ya CRDB imekuwa na utaratibu wa kufuturisha na kutoa futari kila mara kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

“Tumekuja katika kituo hiki ili kutoa futari na daku ikiwa ni sehemu ya kutekeleza maelekezo ya Dini ya Kiislamu yanayotuelezea umuhimu wa kufuturisha watu kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhan hususani kwa watu wasio na uwezo wa kupata Futari”,amesema Pamui.

“Huu ni utaratibu ambao Benki ya CRDB imekuwa ikiufanya mara kwa mara lakini kwa heshima ya watoto wa vituo vya kulelea watoto yatima, Benki ya CRDB imeona ni vyema Futari hiyo tuipeleke moja kwa moja kwenye vituo licha ya wananchi wengine wakiwemo Wateja wa Benki ya CRDB na wasio wateja, Waislamu na ambao siyo Waislamu wanafuturishwa kwenye maeneo mbalimbali kwa lengo la kuleta mshikamano nchini, upendo,amani na furaha kwa jamii”,ameeleza Pamui.

Kwa upande wake, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha kulelea watoto yatima Mjini Shinyanga ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’, Bi. Ayam Ally Said ameishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwasaidia watoto katika kituo hicho akibainisha kuwa watu wengine wanapaswa kuiga benki hiyo.

“Tunawashukuru na kuwapongeza Benki ya CRDB kwani mara kwa mara wamekuwa wakitusaidia hivyo ushirikiano huu unatupa nguvu. Hatujawahi kuwaandikia barua ya kuwaomba waje lakini wamekuwa wakifika hapa, walituletea Mashuka, chakula na leo wameleta Futari kwa ajili ya watoto hawa”,amesema Bi. Ayam.

Mbali na kuishukuru serikali kwa ushirikiano inaowapatia, Bi. Ayam pia ametumia fursa hiyo kuiomba Benki ya CRDB na wadau wengine kuwasaidia kujenga walau darasa moja kwa ajili ya shule ya Chekechea/Nursery ambayo itatumiwa na watoto yatima waliopo kituoni hapo na wale walio nje ya kituo ili kuendelea kuwasaidia zaidi watoto yatima.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Said Pamui akizungumza leo Jumamosi Mei 8,2021 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Futari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kutii maelekezo ya Dini ya Kiislamu yanayoelekeza umuhimu wa kufuturisha watu kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Katikati ni  Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha kulelea watoto yatima Mjini Shinyanga ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’, Bi. Ayam Ally Said akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney (kulia). Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Said Pamui akizungumza leo Jumamosi Mei 8,2021 wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Futari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha kulelea watoto yatima Mjini Shinyanga ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’, Bi. Ayam Ally Said akizungumza wakati Benki ya CRDB ikitoa Futari kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika Kituo hicho. Kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui. Wa kwanza kulia ni Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akifuatiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Luther Mneney
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kituo cha kulelea watoto yatima Mjini Shinyanga ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’, Bi. Ayam Ally Said akiishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kusaidia watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddi akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Futari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

 Bidhaa zilizotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Futari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.

 Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Said Pamui (katikati) akijiandaa kukabidhi Futari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Said Pamui akikabidhi Tende kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi , Said Pamui (wa tatu kulia) akikabidhi Futari kwa ajili watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la kukabidhi Futari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney (kulia) akikabidhi bidhaa kwa ajili kuandalia futari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga.
Zoezi la kukabidhi Futari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Zoezi la kukabidhi Futari kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga likiendelea.
Sehemu ya Watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima ‘Shinyanga Society Orphanage Centre’ kilichopo Bushushu kata ya Lubaga Manispaa ya Shinyanga wakiomba Dua baada ya kupokea Futari kutoka Benki ya CRDB.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post