Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Tanzia : MC DICKSON MITUNDWA AFARIKI DUNIA

 

Mshereheshaji (MC) Dickson Mitundwa mkazi wa Shinyanga amefariki dunia usiku wa kuamkia leo

***

TANZIA TANZIA

Kwa masikitiko makubwa kabisa Uongozi wa KISIMA CHA MAFANIKIO unawatangazia kifo cha Mc Dickson Mitundwa kilichotokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Mei 10,2021.

Ikumbukwe Marehemu alisafiri kutoka Shinyanga tarehe 07 na kufika Dsm tarehe 08 mchana kwa ajili ya kuja kumzika baba yake mzazi.

Alifanikiwa kumzika tarehe hiyo hiyo jioni akisindikizwa na baadhi yetu wana KCM huko makaburi ya Kisarawe.

Kesho yake asubuhi tarehe 09.05.2021 alifanikiwa  kushiriki kisomo na dua kwa marehemu baba yake na kumalizia na kikao cha familia akiwa na nduguze wa baba pamoja na mama yao mjane hukohuko Kisarawe.

Marehemu alipanga kurejea mkoani  Shinyanga siku ya leo Jumatatu lakini ghafla saa 5 Usiku jana hali ilibadilika na ndani ya sekunde chache akajisikia kukosa nguvu, na kukimbizwa haraka sana Hospitali, lakini pamoja na juhudi za madaktari ilishindikana kuokoa maisha yake na kufariki dunia.

Mwili wa marehemu Mc Dickson Mitundwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kusubiri mipango ya mazishi.

Tutaendelea kuwapa taarifa za msiba baada ya kikao asubuhi hii kitakachofanyika ukweni Mombasa ila kwa sasa tunaomba utulivu utawale na kama ilivyo ada mwanachama anapofariki , tunatoa rambirambi kwa familia yake kuanzia sh 10,000 na kuendelea.

Mtunza Hazina Christina Matai ndiye mpokea rambirambi na aina yoyote ya mchango na atatuongoza kwa hilo.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA

JINA LAKE LIHIMIDIWE

MC TEN

KATIBU  MKUU - KCM.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com