Kampuni ya Uzalishaji na Uuzaji wa dawa za asili maarufu Faraja Natural Herb Kigoma inashiriki Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.
Akizungumza leo na Malunde 1 blog iliyotembelea Banda la Faraja Natural Herb Kigoma, Dkt. Faraja Peter amesema wanashiriki Maonesho hayo yanayofanyika kuanzia Mei 24,2021 hadi Mei 30,2021 ili kuonesha na kuuza dawa za asili wanazozalisha kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu kwa kutumia mimea,mizizi,majani na matunda.
“Tunatibu magonjwa kwa kutumia miti shamba ambayo imetumiwa na mababu zetu na dawa hizi hazina kemikali yoyote na zina virutubisho vya kila aina ambavyo ni pamoja na lishe,tiba na kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali”,ameeleza Dkt. Faraja.
Amewakaribisha wananchi kutembelea banda la Faraja Natural Herb Kigoma ili kujipatia dawa za asili na wanaweza kuwasiliana naye kwa simu namba 0766102264 au 0764465691.
Muonekano wa sehemu ya Banda la Kampuni ya Uzalishaji na Uuzaji wa dawa za asili maarufu Faraja Natural Herb Kigoma kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama.
Dr. Faraja Peter kutoka Kampuni ya Uzalishaji na Uuzaji wa dawa za asili maarufu Faraja Natural Herb Kigoma akionesha dawa za asili kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama
Dr. Faraja Peter kutoka Kampuni ya Uzalishaji na Uuzaji wa dawa za asili maarufu Faraja Natural Herb Kigoma akionesha dawa za asili kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama
Dr. Faraja Peter kutoka Kampuni ya Uzalishaji na Uuzaji wa dawa za asili maarufu Faraja Natural Herbal akiwaeleza wananchi waliotembelea banda la Faraja Natural Herb Kigoma dawa za asili kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama
Dr. Faraja Peter kutoka Kampuni ya Uzalishaji na Uuzaji wa dawa za asili maarufu Faraja Natural Herb Kigoma akiwaeleza wananchi waliotembelea banda la Faraja Natural Herb Kigoma dawa za asili kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama
Wananchi wakiwa kwenye banda la Faraja Natural Herb Kigoma wakiangalia dawa za asili kwenye Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama
Sehemu ya dawa za Faraja Natural Herb Kigoma
Social Plugin