Meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akiwakabidhi watoto yatima futari katika kituo cha Kahama Peace Ophanage Center
Meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui akimkabidhi tende mtoto, Abbu Malik (5) kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa katika Kituo cha Kahama Peace Ophanage Center
Sheikh Alhaj Omary Damka akimkabidhi mfuko wa unga wa ngano Saada Hamis anayelewa katika kituo hicho ikiwa ni mmoja misaada iliyotolewa na benki ya CRDB.
Bi Mariamu Missana mfadhili wa Kituo cha Kahama Peace Ophanance Center akipokea futari kutoka kwa meneja wa benki ya CRDB kanda ya Magharibi Said Pamui.
Mtoto Abbu Malik (5) akiwaombea dua viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu walioambatana na maafisa wa benki ya CRDB Kanda ya Magharibi kwa ajili ya kutoa futari katika kituo hicho.
***
Na Salvatory Ntandu - Kahama
Benki ya CRBD Kanda ya Magharibi imetoa futari kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Kahama Peace Ophanage Center kilichopo katika mtaa wa Mhungula Manispaa ya Kahama ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya dini ya kiislamu ya kusaidia watu wenye uhitaji katika jamii hususani katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Akikabidhi futari hiyo leo Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui amesema kuwa kila mwaka katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani benki ya CRDB imekuwa ikitoa misaada mbalimbali ya futari kwa watu wenye mahitaji kama vile wazee, wagonjwa, watu wenye ulemavu na watoto yatima.
“Mwenye Mungu ameagiza sisi wanadamu kutenda matendo mema katika mwezi mtukufu wa Ramadhani,hususani kuwakirimia wajane, wagonjwa, wazee na mayatima hivyo watu wengine wenye uwezo wa kuwasaidia wahitaji wanapaswa kuiga mfano wa benki ya CRDB kwa kuwasaidia watoto yatima ambao wanahitaji uangalizi wa karibu,”alisema Pamui.
Pamui ameahidi benki ya CRDB kuendelea kushiriana na uongozi wa kituo hicho ili kuhakikisha kero mbalimbali zinazowakabili zinatatuliwa na zile ambazo zipo nje ya uwezo wao atazipeleka kwa mamlaka husika ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Awali akipokea msaada huo kwa niaba ya uongozi wa kituo hicho shekhe wa wilaya ya Kahama Alhaj Omary Damka ameishukuru benki ya CRDB kwa kutoa futari hiyo kwa watoto yatima kwani imewapa faraja kwa na kuiona bado jamii inawapenda na kuwathamini.
“Benki ya CRDB Kuwafuturisha watoto yatima katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kujipatia thawabu kutoka kwa mwenyezi Mungu niwaombe msikate tama endeleeni kuwasaidia wahitaji mbalimbali katika jamii,”alisema Shekhe Damka.
Kwa upande wake mfadhili mkuu wa kituo hicho, Bi Maimuna Missana Matembe amesema kuwa watoto hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo chakula mavazi na malazi na kutoa rai kwa wadau wengine kuiga mfano wa benki ya CRDB kwa kuwapatia misaada mbalimbali ili kuwawezesha kujikimu.
“Kituo chetu kinawatoto yatima wapato 25 wenye umri kuanzia miezi mitatu hadi miaka 12,ambao wanalelewa hapa na akinamam ambao wanajitolea kwa hali na mali,tunaomba kusaidiwa kujengewa uzio wa nyumba wanazolala watoto wetu ili kuongeza usalama hususani nyakati za usiku kutokana na eneo letu kutokuwa na uzio,”alisema Missana.
Social Plugin