Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed akionesha bidhaa original anazotumia kupamba maharusi kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wataalamu wa Urembo maarufu Kahama Glamour Beauty Salon wameshiriki Maonesho ya Wajasiriamali na Wawekezaji Kahama yanayofanyika katika Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kilichopo Nyihogo Mjini Kahama.
Akizungumza na Malunde 1 blog iliyotembelea banda lake, leo Alhamis Mei 27,2021 Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed amesema wanashiriki maonesho hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya GS1 Tanzania ili kutangaza biashara na kazi wanazofanya pamoja na kujifunza kutoka kwa wajasiriamali wengine.
“Kahama Glamour Beauty Salon tunapamba maharusi, tunasuka nywele aina zote, tunauza bidhaa mbalimbali za urembo, tunakodisha nguo za harusi, tunafanya Decoration ya Paper Flower katika matukio mbalimbali,tunauza mapambo ya ndani kama vile saa za ukutani pia tunafundisha kuhusu kazi tunazofanya”,amesema Sharifa
Kahama Glamour Beauty Salon inapatikana Nyihogo Kahama karibu na Haliwa Restaurant , mawasiliano 0753846701 Instagram @Kahama Glamour Beauty Salon
Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed akionesha picha ya ukutani kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed akionesha gauni la harusi kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama
Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed akionesha Paper Flower Decoration ambazo anatengeneza mwenyewe kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama
Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed akionesha saa ya ukutani kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama
Mkurugenzi wa Kahama Glamour Beauty Salon, Bi. Sharifa Mohammed akionesha saa ya ukutani kwenye maonesho ya wajasiriamali na wawekezaji Kahama.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Soma pia:
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin