Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza na watumishi katika mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Taifa cha Utalii jijini Arusha ambapo amewataka watumishi kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ili kufikia malengo yaliyowekwa.
Katibu wa Baraza, Shaha Nampeha akizungumza na watumishi ambapo amewataka watumishi hao kufanyakazi kwa mashikamano mahali pa kazi.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Lusius Mwenda akiwasilisha mada na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kiutumishi wakati wa Mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Arusha.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Ludovick Nduhiye akizungumza wakati wa mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi ambapo amewataka watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa katika mkutano huo.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifuatilia maelekezo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akizungumza na watumishi wa Wizara hiyo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi unaofanyika jijini Arusha.
Mwenyekiti wa TUGHE, Anthony K. Tibaijuka akizungumza wakati wakati wa Mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi ambapo amewataka watumishi kufanya kazi kwa bidii ili kukuza na kuendeleza sekta ya maliasili na utalii.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wa Wizara hiyo katika Baraza la Wafanyakazi la 28 linalofanyika leo jijini Arusha.
Social Plugin