WAKULIMA WATAKIWA KUBADILI FIKRA NA KUANZA KULIMA KILIMO CHA UMWAGILIAJI


Mhandisi Christpher Mashalla 

Ili kuhakikisha wakulima mkoani Shinyanga wanajikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini wakulima wametakiwa kubadili fikra na kuanza kulima kilimo cha umwagiliaji.

Wito huo umetolewa  leo Mei 20, 2021 na Mhandisi wa kilimo na
umwagiliaji mkoa wa Shinyanga,mhandisi Christopher Mashalla wakati akizungumza na Malunde 1 Blog ofisini kwake.

Ameeleza kuwa zaidi ya Sh. Bilioni 4 zinahitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Skimu ya umwagiliaji katika kata ya Nyida halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Shilingi milioni 100 kwa ajili ya ukarabati wa mradi wa Skimu ya umwagiliaji Mwamalili katika halimashauri ya manispaa ya Shinyanga.

Mashalla amsema kuwa baada ya kuanzisha ofisi ya kilimo na
 umwagiliaji mkoa wa Shinyanga wameweka mkakati madhubuti wa kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa wananchi kulima kilimo cha umwagiliaji pamoja na kuainisha maeneo maalumu watakayojenga Skimu za umwagiliaji katika mkoa wa shinyanga

Aidha  amesema kuwa iwapo watapata fedha hizo wataweza kujenga na kukarabati miradi hiyo hali itakayo wapa fursa wananchi wengi kuchangamkia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post