Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NGOMA YA NAY WA MITEGO 'MAMA' YAKWAMA BASATA


Wimbo wa Nay wa mitego “Mama” umekwama BASATA kutokana na kukosa vigezo baada ya kukaguliwa.

Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kupitia kaimu katibu mtendaji Matiko Mniko lilitangaza kuwa kuanzia tarehe 1 Mei,2021 wataanza kutumia kanuni za kuzipitia nyimbo mpya za wasanii wote Tanzania kabla ya kupelekwa kwenye vituo vya Redio na Runinga.

Jamatatu mkali huyo wa hip hop alikuwa aachie kazi yake mpya lakini hakufanya hivyo baada ya wimbo huo kukwama kutokana na marekebisho ambayo ameamriwa na baraza kuyafanya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com