Katibu wa baraza la wazee Manispaa ya Kahama Underson Lyimo, akizungumza kwenye kikao cha kutathimini na kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee.
Na Marco Maduhu, Kahama
BARAZA la wazee Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, wamelaani tukio la mauaji ya mzee Mayombo Songo (75) mkazi wa Wendele Manispaa hiyo, ambaye aliuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.
Wazee walipaza kilio hicho jana kwenye kikao cha kutathmini na kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee Manispaa hiyo, kilicho andaliwa na Shirika la TAWLAE ambalo linatekeleza miradi ya kutetea haki za wazee mkoani Shinyanga.
Katibu wa Baraza la wazee Manispaa ya Kahama Underson Lyimo, alisema mauaji ya wazee yalikuwa yamekwisha, lakini mwaka huu yameanza kuibuka upya, na kuitaka Serikali pamoja na vyombo vya usalama kuyadhibiti ili yasiendelee kutokea.
"Baraza la wazee Manispaa ya Kahama, tunalaani mauaji ya mzee mwezetu ambaye aliuawa kwa kukatwa mapanga usiku akiwa amelala nyumbani kwake na watu wasiojulikana, tunaitaka Serikali na vyombo vya usalama kuyadhibiti ili yasitokee tena,"alisema Lyimo.
Naye Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Polisi wilayani Kahama Elias Sikanda, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Polisi wilayani humo, alithibitisha kutokea kwa mauaji ya mzee huyo, na kubainisha kuwa bado wanawasaka watu waliohusika na mauaji hayo.
Pia alisema Jeshi la Polisi wamejipanga vyema kudhibiti mauaji ya wazee yasitokee tena, ambapo wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara kutoa elimu kwa wananchi, juu ya kuthamini wazee na kuacha kutekeleza mauaji dhidi yao.
Naye Afisa miradi kutoka Shirika hilo la TAWLAE Winie Hinaya, alisema jamii inapaswa kuwalinda wazee pamoja na kuwatunza, na siyo kuwaona kama mikosi kwao huku wakiwatuhumu ni washirikina, na kuwa uwa kwa mapanga, kitendo ambacho ni ukeukaji wa haki za binadamu.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Katibu wa baraza la wazee Manispaa ya Kahama Underson Lyimo, akizungumza kwenye kikao cha kutathimini na kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee.
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Polisi wilayani Kahama Elias Sikanda, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Polisi wilayani humo kwenye kikao hicho.
Afisa miradi kutoka Shirika la Tawlae Winie Hinaya, akizungumza kwenye kikao hicho na kuelezea mradi wao wa kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee.
Wazee wakiwa kwenye kikao cha kutathimini na kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee Manispaa ya Kahama.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea cha kupanga mikakati ya kutokomeza matukio ya ukatili dhidi ya wazee kikiendelea.
Picha ya pamoja baada ya kikao kumalizika.
Na Marco Maduhu, Kahama.
Social Plugin